ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA MOTO UMEWAKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 15 March 2024

ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA MOTO UMEWAKA


Droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali imepangwa muda mfupi uliopita huku Arsenal ikipewa Bayern Munich na Manchester City vigogo Real Madrid.



Droo hiyo imefanyika leo Ijumaa Machi 15, 2024 huko Nyon, Uswisi ambapo mechi ya kukata na shoka inatazamiwa kuwa kati ya Mabingwa wa Kihistoria Real Madrid dhidi ya bingwa mtetezi, Manchester City.


Mechi nyingine ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki ni ile ya Arsenal ambayo inatafuta ubingwa wake wa kwanza, ikipangwa kuvaana na Bayern Munich.


Mechi hizo zinatarajiwa kupigwa kati ya Aprili 9/10 na marudio Aprili 16/17, mwaka huu.


Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kupigwa Juni Mosi, kwenye Uwanja wa Wembley jijini London, Uingereza.


ROBO FAINALI.
• Arsenal v FC Bayern Munich
• Atletico Madrid v Borussia Dortmund
• Real Madrid v Manchester City
• PSG v FC Barcelona


NUSU FAINALI
Mshindi: Arsenal/ Bayern v Real/ Man City
Mshindi: Atletico/ Borussia v PSG/ Barcelona.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso