DIWANI AFARIKI GHAFLA BUNDA, MWILI KUFANYIWA UCHUNGUZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 15 March 2024

DIWANI AFARIKI GHAFLA BUNDA, MWILI KUFANYIWA UCHUNGUZI


Diwani wa Kisorya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Amos Ndaro amefariki dunia.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Charles Manumbu amethibitisha kutokea kwa kifo hicho usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2024.

Manumbu amesema kifo cha diwani huyo ni cha ghafla, kwani hadi jana hakuwa na tatizo lolote la kiafya.

"Nimeongea naye jana, kuna mambo alitaka ufafanuzi lakini pia alikuwa na vikao kwenye kata yake ambavyo alivifanya hadi mwisho. Ninachoweza kusema mwenzetu amelala na Mungu ndiye anapanga saa ya kumchukua mja wake" amesema.

Amesema mwili wa marehemu umepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi na kwamba baada ya uchunguzi watajua kwa undani chanzo cha kifo hicho na taratibu za mazishi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso