ATOLEWA SKRUBU (SCREW) KWENYE MAPAFU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 23 January 2024

ATOLEWA SKRUBU (SCREW) KWENYE MAPAFU

Mtoto mwingine ametolewa Skrubu (Screw) kwenye mapafu yake kwa kutumia kifaa chenye kamera na kwenda kuinasa na kisha kuitoa ambayo alikua akichezea kinywani mwake wakati akiwa shuleni na hatimaye kumpalia na kisha kukwama na kushindwa kutoka.


Bingwa wa Magonjwa ya Maparu a Mfumo wa Upumuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mwanaada Kilima anasema mtoto huyo alipaliwa na skurubu hiyo siku nne zilizopita ambayo iliyoingia kwenye mapafu yake na kusababisha kukohoa sana na kushindwa kutoka kwa nia ya kawaida.

Bw. Msafiri Chatanda, mzazi wa mtoto huyo amewashukuru watoa huduma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa jitihada kubwa waliyofanya tang alipofikishwa hospitali hapo na kufanikisha kutoa skurubu hiyo.

Bw. Chatanda amewaasa wazazi kuwa watoto wamekuwa na desturi ya kuchezea vitu lakini hakuna mzazi anaangaika kumkumbusha moto madhara yake na kuona kuwa ni kitu cha kawaida.

Katikati ya mwezi huu, Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili lilifanikiwa kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la moto mwenye umri wa miaka mitano.

Aidha, mapema jana, Daktari wa Magonjwa ya Mapatu na Mfumo wa Upumuaji, Dkt. Hedwiga Swai akishirikiana na wenzake walifanikiwa kumtoa mama mwenye umri wa miaka 53, ganda la pipi kwenye pafu lake la kushoto alilodumu nalo kwa miaka 11 kwa kutumia kifaa maalum chenye kamera kilichopelekwa moja kwa moja hadi lilipo na kulinasa na kisha kulitoa.

Chanzo;Millard ayo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso