WANNE WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KOSA LA KUUA MME NA MKE-SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 22 September 2023

WANNE WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KOSA LA KUUA MME NA MKE-SHINYANGA


Washtakiwa Wanne waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga wamehukumiwa Kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kuuwa kwa kukusudia watu wawili ambao ni mtu na mke wake.


Hukumu hiyo imetolewa Septembe 21, 2023 katika Mahakama kuu kanda ya Shinyanga mbele ya Jaji wa Mahakama hiyo Jaji Seif Mwinshehe Kulita ambapo amesema kuwa baada ya kusikiliza mashahidi saba wa upande wa Jamhuri Ushahidi huo pasipo kaacha shaka kuwa watu hao walikusudia kufanya mauaji hayo.


Tukio hilo la mauaji lilitokea katika Kijiji cha Masengwa halmashauri ya Shinyanga Mwaka 2019 baada ya kaka wa Marehemu kukodi washtakiwa namba 2 hadi 4 kwa kuwalipa ujira wa Shilingi milioni 1 na laki 2 ili wakatimize hitaji la moyo wake kwa kuwauwa kaka yake pamoja na mke wa kaka yake ambapo Ushahidi umeoneha kuwa waliuwawa kwa kukatwa na Mapanga pamoja na shoka vitu ambavyo vilikutwa eneo la tukio.


Jaji Kulita amesema kuwa katika Ushahidi wa shahidi na 5 ulionesha kuwa walikwenda eneo la tukio na kufanya uchunguzi ambapo mshitakiwa wa nne alikiri kushiriki kwa kulipwa ujira wa sh. Laki 4 ambazo zilikuwa zimefichwa chini ya ardhi.


Aidha katika Ushahidi wa shahidi wa 3, 4, 6 na 7 umeonesha na kutoacha shaka kuwa washtikiwa hao walifanya kosa hilo kwa kukusudia baada ya kupewa pesa ili Kwenda kutekeleza mauaji hayo nyumbani kwa marehemu.


Katika shitaka hilo namba 14 la mwaka 2022 washtakiwa wakiongozwa na Salawa Ndelema aliyewalipa milioni 1 na laki 2 kwenda kutekeleza maauaji ya kuumua kaka yake aitwaye Mayala Ndelema na Mkewe Nyamizi Mserengeti ambapo fedha hizo zilitumika pia kununua panga pamoja na shoka.


Katika maelezo yake Jaji Kulita amesema washtakiwa hao walipewa nafasi ya kujitetea ambapo kila mmoja alieleza jinsi tukio hilo lilivyomkuta ambapo maelezo yao hayakuwa na mashiko mbele ya Mahakama hiyo .


Ushahidi umeweka wazi kuwa mshitakiwa no 1 Salawa Ndelema ambaye ni mdogo wa Marehemu Mayala Ndelema aliwakodisha watuhumiwa namba 2 3 na 4 kwa sababu alikuwa na mgogoro wa ardhi na kaka yake huyo huku akimtuhumu shemeji yake Marehemu Nyamizi Mserengeti kuwa ni mchawi na amekuwa akimloga


Jaji kulita baada ya kupitia Ushahidi wa mashahidi saba kutoka Upande wa jamhuri ambao haukucha shaka wamkutwa na hatia ya kuuwa kwa kukusudia na kuwapa adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wote wanne ambao ni Salawa Ndelema, Mayala Charles, Shija Ngelanija na Emanuel Manoni.


Kesi hiyo upande wa Jamhuri ilikuwa na Mawakili watatu wakiongozwa na Shani,Wampumbulya,Upendo Mwakimonga na Magoti Nyamunyaga huku upande wa utetezi ukiwa na mawakili wanne wakiongoza na Wakili Geofrey Tuli.


Chanzo:Malunde 1 blog

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso