OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATAJA MFUMKO WA BEI KUSHUKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 9 August 2023

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATAJA MFUMKO WA BEI KUSHUKA


Kupungua kwa bei katika baadhi ya bidhaa za chakula na vinywaji baridi kumefanya mfumuko wa bei wa Taifa kushuka hadi kufikia asilimia 3.3 katika mwaka ulioishia Julai 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.6 katika mwaka ulioishia Juni 2023.


Hii ikiwa na maana kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Julai, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Juni, 2023.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonyesha kupungua bei kwa mwaka ulioishia Julai, 2023 ni ngano kutoka asilimia 4.8 hadi asilimia 3.1, mchele kutoka asilimia 17.0 hadi asilimia 11.4, mahindi ulitoka asilimia 22.9 hadi asilimia 7.2.


“Unga wa ngano ulipungua kutoka asilimia 1.8 hadi asilimia 1.5, unga wa mahindi ulipungua kutoka asilimia 30.5 hadi asilimia 16.5, mikate na vyakula vingine vya kuoka kutoka asilimia 11.6 hadi asilimia 11.1, samaki wabichi kutoka asilimia 8.9 hadi asilimia 6.1,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso