KLABU YA SIMBA YATUHUMIWA KUDHALILISHA WENYE UALBINO SIKU YA SIMBA DAY - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 9 August 2023

KLABU YA SIMBA YATUHUMIWA KUDHALILISHA WENYE UALBINO SIKU YA SIMBA DAY


Chama cha watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wameitaka klabu ya Simba kuomba radhi kwa tukio waliloita la udhalilishaji.


Tukio hilo lilitokea Agosti 6, 2023 kwenye sherehe ya tamasha la siku ya Simba yaliyofanyika uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini hapa kwa kumpandisha mtu mwenye ulemavu wa ngozi akiwa amevishwa taulo ya watoto (baby diaper).


Msemaji wa Simba Ahmed Ally alipoulizwa kwa simu leo, amesema wamesikia na wapo tayari kufanya hivyo.


“Wamesema tuombe radhi? Basi sawa. Kwa sasa tuko busy na mechi ya kesho, akili yetu yote ipo kwa kwa ajili ya kesho. Haya mambo mengine tukianza kujibu tutavuruga utaratibu. Nitamuuliza CEO tuone tunafanya nini,” amesema.


Akizungumza leo Jumatano Agosti 9, 2023 jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa TAS, Godson Mollel amesema tukio hilo ni la pili kwa Simba kulifanya ambalo la kwanza lilikuwa Agosti 8, 2022 waliingia na jeneza ambalo lilimbeba mtu mwenye ualbino.


Amesema vitendo hivyo vinawatweza utu wa watu wenye ualbino nchini na kupelekea kuwepo kwa mijadala mingi katika jamii ikiwemo mitandaoni inaonyesha dhihaka kwa watu hao kinyume na haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso