BASI LA KAMPUNI YA AM SAFARI LAPATA AJALI MWENDAKULIMA-KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 21 August 2023

BASI LA KAMPUNI YA AM SAFARI LAPATA AJALI MWENDAKULIMA-KAHAMA

Gari la abiria aina ya Scania Kampuni ya AM Safari linalofanya safari zake kutoka Kahama kuelekea Dodoma, limepata ajali eneo la Mizani mjini Kahama mkoani Shinyanga na kujeruhi watu wawili.

 

 Basi la AM Safaris lililopata ajali eneo la Mzani Kahama

Chanzo ajali hiyo kikielezwa kuwa ni Mwendokasi ambapo dereva alishindwa kumudu kona ya kuingia eneo la Mizani.

  

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa shinyanga ACP Janeth Magomi amesema kuwa watu wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama kwa ajili ya Matibabu zaidi.

  

Kamanda Magomi amesema licha ya uzembe wa Dereva lakini pia gari hilo ni bovu na limezuiliwa kuendelea kutoa huduma, huku akiwataka Wamiliki na Wasafirishaji kuzingatia Sheria za Usalama barabarani ikiwemo kuhakiki Magari yao kabla ya kuanza safari.


CHANZO: MALUNDE 1 BLOG

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso