RAIS MSTAAFU KIKWETE ASEMA KUCHANGANYA DINI NA SIASA NI UVUNJIFU WA AMANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 20 August 2023

RAIS MSTAAFU KIKWETE ASEMA KUCHANGANYA DINI NA SIASA NI UVUNJIFU WA AMANI


Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete amewaonya viongozi wa dini na siasa kutumia dini kwa manufaa yao huku akisema ni hatari kwa amani ya nchi.


Kikwete ameyasema hayo leo Jumapili Agosti 20, 2023 katika uzinduzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Charya Kamageta wilayani Rorya mkoani Mara.


"Natumia nafasi hii kukumbusha kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, kama kuna viongozi wa dini wanaotaka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kama kuna Viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa nawaombeni tuwanyanyapae,”amesema Kikwete.


Kikwete amesema athari ya kuchanganya dini na siasa ni uvunjifu mkubwa amani na utulivu wa Taifa.


“siku ikifika uwanachama wa chama cha kisiasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha kisiasa anachokifuata ndiyo mwisho wa nchi yetu.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso