WAANDISHI HABARI MKOANI KAGERA WAKUMBUSHWA KUENDELE KUANDIKA HABARI ZINAZOLINDA MASLAHI YA TAIFA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 20 May 2023

WAANDISHI HABARI MKOANI KAGERA WAKUMBUSHWA KUENDELE KUANDIKA HABARI ZINAZOLINDA MASLAHI YA TAIFA

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Erasto Siima, amewataka Wanahabari Mkoani humo, kutoshinikizwa na mtu yeyote, kutoa taarifa zisizo sahihi, zinazoweza kuhatarisha amani iliyopo hapa nchini.


Na Mutayoba Arbogast,HUHESO DIGITAL,Bukoba


Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Erasto Siima,akizungumza na washiriki maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari.Kushoto kwake ni mwenyekiti KPC, Mbeki Mbeki

Siima ametoa kauli hiyo, akiwa Mgeni rasmi, katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari, kwa Chama Cha waandishi wa habari,mkoa wa Kagera( Kagera Press Club-KPC) yaliyofanyika katika ukumbi wa Bukoba Coop, uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani humo,19 Mei 2023.


Siku hiyo ya Uhuru wa vyombo vya habari Ulimwenguni huadhimishwa kila mwaka Mei 3 (KPC ilisogeza maadhimisho hayo mbele kutokana na sababu nje ya uwezo wao) ili kuchochea uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari,na pia kuwakumbusha viongozi wakuu wa nchi mbalimbali juu ya umuhimu wa haki za binadamu.


DC Siima, amesema kuwa, wakati waandishi wa habari wakiadhimisha siku hiyo, wanatakiwa kutoshinikizwa na mtu yeyote, kwani madhara yake ni makubwa, ikiwemo kukosekana kwa amani,badala yake watoe taarifa sahihi na zenye ukweli.


Aidha, mkuu huyo wa wilaya amewasihi wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kuwa wanarusha vipindi  muhimu kwa maendeleo ya jamii kwa muda unaowazesha wasikilizaji kufuatilia, na siyo wakati usio rafiki kwa wasikilizaji, hali kadhalika habari hizo zichapwe kwenye kurasa pendwa,ili kurahisisha kuchochea shughuli za maendeleo.


Amewashukuru wanachama wa Kagera Press Club, pamoja na waandishi wa habari wengineo, kwa namna walivyotoa ushirikiano  kwa Serikali, katika kutoa habari pamoja na kuwa mstari wa mbele, kufuatilia matukio mbali mbali yanayoutangaza mkoa huo, huku akiahidi kuwapa ushirikiano mkubwa.


Mbeki Mbeki, ambaye ni mwenyekiti  wa Chama cha Waandishi habari mkoa wa Kagera, ametumia nafasi hiyo kuwaomba waajiri wa vyombo vya habari mkoani humo kuwajali na kuwathamini wafanyakazi wao pindi wanapopatwa na matatizo wakiwa kazini.


Maadhimisho hayo yamewashirikisha wanafuzi 50 kutoka shule za sekondari tano kutoka manispaa ya Bukoba ambazo ni Kashai,Bilele,Bukoba,Rumuli na Hamugembe,ambapo kila shule iliwakilishwa na wanafunzi kumi,kwa lengo la kupata ufafanuzi juu ya Haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.

Peter Matete ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wa kujitegemea, kanda ya Kagera,alitoa ufafanuzi juu ya kauli mbiu ya mwaka huu isemayo, 'Mustakabali wa Haki: Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki nyinginezo za kibinadamu',ambapo pia wanafunzi walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao.

Wandishi wa habari wanachama wa KPC, katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Bukoba

Wanafunzi  katkka picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Bukoba



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso