JNHPP KUANZA KUZALISHA UMEME - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 31 May 2023

JNHPP KUANZA KUZALISHA UMEME

Serikali imetangaza kuwa, wiki moja ijayo kina cha maji katika bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) litakuwa na uwezo wa kuanza kuzalisha umeme.


Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 31, 2023 na Waziri wa Nishati, Januari Makamba wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka 2023/24 ambayo ameliomba Bunge lipitishe jumla ya Sh3.048 trilioni.

Waziri Makamba amesema kuwa ujazo wa maji uliofikiwa katika Bwawa hilo ni mita za ujazo 163, lakini kiwango kinachotakiwa bado mita za ujazo mbili.

“Mheshimiwa Spika, ninafurahi kulitaarifu Bunge lako kuwa, wiki ijayo hata tukiamua kuanza uzalishaji wa umeme tunaweza kwani kiwango cha chini cha uzalishaji maji tumebakiza mita za ujazo mbili tu,” amesema Makamba.

Hata hivyo Waziri amesema kuwa uzalishaji wa umeme utakaoanza rasmi katika mwaka huu wa fedha, utaingizwa katika gridi ya Taifa mwakani sambamba na umeme wa jua.

Habari zaidi 

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/bwawa-la-nyerere-kuanza-uzalishaji-umeme-4253028

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso