CHRISTINA MNDEME ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 26 February 2023

CHRISTINA MNDEME ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa wakuu wa mikoa mitatu ya Shinyanga, Tanga na Songwe.

 

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme


Wakuu wa mikoa wapya walioteuliwa ni Christina Mndeme ambaye anakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga huku aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Francis Michael ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.


Christina Mndeme anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ambae alichaguliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.


Aidha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba amehamishiwa Mkoa wa Tanga, huku aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Omary Mgumba uteuzi wake ukitenguliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso