AFIKISHWA MAHAKAMANI AKIWA NA KOBE 998, MAGAMBA 10 YA KOBE, MKIA WA NYATI ADAI ANAENDA KUTIBU WATU UKIMWI AMEOTESHWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 3 February 2023

AFIKISHWA MAHAKAMANI AKIWA NA KOBE 998, MAGAMBA 10 YA KOBE, MKIA WA NYATI ADAI ANAENDA KUTIBU WATU UKIMWI AMEOTESHWA

Mkazi wa Kijiji cha Nyarukoru, mkoani Mara, Matimba Washa (28), ameshtakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Butiama kwa makosa matatu likiwamo la kukutwa na kobe 998, magamba 10 ya kobe, ngozi ya Nyati na mkia wa Nyumbu, vyote vikiwa na thaman ya Sh168 milioni.


Mshtakiwa huyo akidai ameoteshwa na mapepo kuwa nyara hizo za Serikali ni tiba ya magonjwa kama vile ukimwi, seli mundu na magonjwa ya zinaa.


Washa aliwaambia Polisi katika mahojiano kuwa dawa yake ina uwezo wa kutibu magonjwa hayo. Pia alitoa maelezo hayo mahakamani na kuwaomba washitaki wake wamletee mahakamani hapo mtu yeyote mwenye ugonjwa mmojawapo ili awathibitishie uwezo wa dawa hizo.


Kijana huyo amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Julieth Semkiwa, leo Alhamisi Februari 2 2023.


Mwendesha mashtaka, wakili wa serikali Gaston Kayombo amesema mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa makosa matatu ya kukutwa na nyara za serikali pamoja na uhujumu uchumi.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso