AKAMATWA NA WANANCHI AKITOROSHA MTOTO WA BOSS WAKE STENDI YA NYEGEZI MWANZA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 3 February 2023

AKAMATWA NA WANANCHI AKITOROSHA MTOTO WA BOSS WAKE STENDI YA NYEGEZI MWANZA


Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limeanza uchunguzi wa tukio la mtoto aliyetambuliwa kwa jina la Hamisa Mung'ong'o (10) anayedaiwa kukamatwa na wasamalia wema katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza katika harakati za kutoroka na mtoto wa mwajiri wake kwenda mkoani Mbeya.


Taarifa ya mtoto huyo ilisambaa kuanzia jana Jumatano Februari Mosi mwaka huu katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha binti huyo akihojiwa na mwanamke ambapo alinukuriwa akijibu kuwa kichanga hicho ambacho ni cha mwajiri wake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema katika mahojiano binti huyo alidai kusafirishwa kutoka kwa wazazi wake mkoani Mbeya na mwalimu wa Shule ya Msingi Ilendeja iliyoko Kisesa wilayani Magu mkoani hapa kwa lengo kuja kumsaidia kazi huku kukiwa na ahadi ya kumsomesha jambo ambalo halikufanyika.
No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso