WATU NANE WAFARIKI KWA KUPIGWA RISASI KWENYE SHEREHE YA BIRTHDAYPART USIKU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 30 January 2023

WATU NANE WAFARIKI KWA KUPIGWA RISASI KWENYE SHEREHE YA BIRTHDAYPART USIKU


Watu wenye silaha wamewauwa wageni wanane baada ya kulifyatulia risasi kikundi cha watu waliokuwa wakisherehekea siku ya kuzaliwa katika mji wa jimbo la Eastern Cape, nchini Afrika Kusini, polisi imesema.


Watu wawili wenye bunduki waliingia kwenye eneo la nyumba hiyo Jumapili usikulililopo katika Gqeberha, zamani likiitwa Port Elizabeth, na kuwapiga risasi wageni kiholela, imesema taarifa ya polisi.


Mmiliki wa nyumba alikuwa ni miongoni mwa wale waliouawa, huku watu wengine watatu wengine wakijeruhiwa.


Waziri wa polisi, Bheki Cele, na mkuu wa polisi, Fannie Masemola, wanatarajiwa kuongoza ujumbe kuelekea kwenye eneo la tukio Jumatatu.


Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa na uchunguzi umeanzishwa kuhusu shambulio hilo, zimesema taarifa za vyombo vya habari nchini humo.


CHANZO:BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso