WATEULE WA RAIS WASHINDWA KURIPOTI MAENEO YAO YA KAZI, WAHOJIWA NA POLISI KWA DAKIKA 50 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 30 January 2023

WATEULE WA RAIS WASHINDWA KURIPOTI MAENEO YAO YA KAZI, WAHOJIWA NA POLISI KWA DAKIKA 50


Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Japheth Maganga amesema kwa sasa hawezi kutoa sababu kwanini hajaripoti wilaya aliyopangiwa ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera huku akihojiwa na Jeshi la Polisi, mkoani Tanga.


Waliomhoji Maganga ni Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanga wakitumia zaidi ya dakika 50.


Bado Polisi hawajaweka wazi sababu za mahojiano hayo.


Maganga na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa wiki iliyopita na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wakuu wa wilaya lakini wakati wenzao wakiapishwa kwenye maeneo yao leo Jumatatu, Januari 30, 2023 wao wapo jijini Tanga wakiongoza mkutano wa viongozi wakuu wa CWT.


Ulaya aliteuliwa kuwa DC wa Mbogwe, Mkoa wa Geita ambapo wenzake wanaapishwa leo Jumatatu na Mkuu wa Mkoa huo, Martin Shigela.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso