WALIKUWA WANATUKANANA VIPIMO VILIKUWA HAVIJAISHA MUDA WAKE, NI WAUUGUZI WALIOSAMBAA MTANDAONI WAKITUKANANA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 12 January 2023

WALIKUWA WANATUKANANA VIPIMO VILIKUWA HAVIJAISHA MUDA WAKE, NI WAUUGUZI WALIOSAMBAA MTANDAONI WAKITUKANANA


Takribani wiki moja tangu kusambaa kwa video ya watumishi wawili wa afya wakibishana juu ya matumizi ya vipimo vilivyosadikika kuisha muda wake, Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimesema kimebaini kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu baina ya watumishi hao.


Kufuatia video hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema watafanya uchunguzi.


Kama hiyo haitoshi, Halmashauri ya Wilaya Uyui ilitangaza kuwasimamisha kazi muuguzi huyo aliyetajwa kwa jina la Rose Shirima na mteknolojia wa maabara aliyetajwa kwa jina la James Chuchu waliokuwa wakifanya kazi katika zahanati ya Ishilimuya Kata ya Bukumbi, ili kupisha uchunguzi.


Taarifa iliyotolewa na TANNA leo Januari 12 imesema kabla ya kuanza kurekodiwa kwa video hiyo, kulikuwepo na lugha za matusi zinazodaiwa kutolewa na James Chuchu kwa Rose Shirima hali iliyofanya muuguzi huyo naye kumjibu kwa lugha isiyo na staha bila ya kufahamu kuwa anarekodiwa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso