KUNDI LA 17 LAONDOKA NGORONGORO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 12 January 2023

KUNDI LA 17 LAONDOKA NGORONGORO

Kundi la 17 lenye jumla ya kaya 34 na watu 179 pamoja na Mifugo 625 leo Januari 12 limeondoka rasmi kutoka eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga.
Idadi hiyo inafanya jumla ya wakazi wa Ngorongoro ambao tayari wameshahamia Msomera mpaka sasa kuwa watu 2629 na mifugo 14132.


Kundi hili ambalo ni la kwanza kuondoka ngorongoro Kuelekea Msomera kwa mwaka huu limejumuisha watu maarufu katika jamii wakiwemo viongozi wa mila wa jamii ya Kimaasai naarufu kama Malaigwanani pamoja na vijana ambao kwa pamoja wameonekana kuwa na tumaini jipya la Maisha yao.


Akiwaaga wakazi hao Mkuu wa Wilaya ya ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala amewahakikishia wakazi hao huduma bora za kijamii ukilinganisha na zile walizo kuwa wakipata Ngorongoro.


CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso