ASHIKILIWA BAADA YA MKE WAKE MZIMBABWE KUFARIKI AKIWA ANAVUJA DAMU MDOMO AKITIBIWA PWANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 12 January 2023

ASHIKILIWA BAADA YA MKE WAKE MZIMBABWE KUFARIKI AKIWA ANAVUJA DAMU MDOMO AKITIBIWA PWANI


MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kutokana na utata wa kifo cha anayedaiwa kuwa mke wake Primrose Matsambire (39) raia wa Zimbabwe .


Primrose amefariki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi januari 11 alipopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kukutwa akiwa anatokwa na damu mdomoni akiwa nyumbani kwake Kiluvya Madukani Wilaya ya Kisarawe.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo alieleza ,aliyegundua marehemu kutokwa damu kwa wingi mdomoni ni msichana wa kazi, baada ya kuona hali hiyo ya marehemu alienda kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kumpeleka katika hospitali ya Tumbi kwa matibabu.


Alisema mume wa marehemu hakuwepo wakati tukio hilo likitokea na kwamba anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano na uchunguzi wa kina wa kifo cha mke wake.


Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Tumbi huku chanzo cha kifo hicho kikiendelea kuchunguzwa.


Chanzo:fullshangwe.co.tz

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso