MKANDARASI AKABIDHIWA MRADI WA UMEME WA BILIONI 6.5 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 30 December 2022

MKANDARASI AKABIDHIWA MRADI WA UMEME WA BILIONI 6.5

Wakala wa nishati vijijini (REA) kanda ya magharibi imemkabidhi mkandarasi mradi wa kusambaza umeme wenye thamani ya zaidi ya shilingi billion 6.5 utakao yafikia maeneo 46 ya pembezoni mwa miji ya Nzega na Tabora.


Makabidhiano ya mradi huo yamefanyika katika ofisi ya TANESCO kanda ya magharibi Mkoani Tabora ambapo meneja uthibiti na ufatiliaji mhandisi Yusufu Ismail amesema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 18 na utawafikia zaidi ya wananchi 2000.


Awali mkandarasi wa mradi huo akitambulishwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora, balozi Dkt. Batilda Buriani amemtaka kuhakikisha anatoa kipaumbele cha nafasi za ajira kwa wakazi wa Tabora pamoja na kuwapa malipo kwa wakati.


Mradi huo wa kufikisha huduma ya umeme pembezoni mwa miji (PERI URBAN) unatekelezwa chini ya mkandarasi wa ndani kupitia kampuni ya OK ELETRICAL SERVICES LTD.


CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso