AACHIWA HURU BAADA YA KUKUBALI KUMUOA ALIYEMBAKA MWANAMKE KIZIWI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 30 December 2022

AACHIWA HURU BAADA YA KUKUBALI KUMUOA ALIYEMBAKA MWANAMKE KIZIWI

Mahakama ya Pakistan ilimwachilia huru Dawlat Khan (25) ambaye ni mtuhumiwa wa ubakaji baada ya kukubali kumuoa binti aliyekuwa amembaka.

Uamuzi huo umetolewa baada ya baraza la wazee kaskazini - magharibi mwa nchi hiyo kuiomba mahakama kuirejesha kesi hiyo kwao ili kutafuta suluhu.


Wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu nchini humo wamepinga suala hilo ambapo wanasema unahalalisha unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.


Dawlat Khan, 25, alihukumiwa mwezi Mei kifungo cha maisha jela na mahakama ya chini katika wilaya ya Buner katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa kwa kumbaka mwanamke kiziwi.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso