WANAFUNZI WA KIKE KUJENGEWA VYUMBA VYA KUJISITIRI SERIKALI YATOA TAMKO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 8 November 2022

WANAFUNZI WA KIKE KUJENGEWA VYUMBA VYA KUJISITIRI SERIKALI YATOA TAMKO

Serikali imeziagiza halmashauri zote kujenga vyumba vya kujisitiri kwa wanafunzi wa kike ili kuwasaidia wakati wakiwa katika hedhi na hivyo kutokosa masomo.


Hayo yamesemwa leo Jumatano Novemba 8, 2022 na Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), David Silinde wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Santiel Kirumba.


Katika swali lake la nyongeza, Santiel amesema kwa kuwa wanafunzi wengi wa kike wamekuwa wakikosa masomo kwa siku 50 kwa mwaka.


Alihoji ni nini ahadi ya Serikali katika madarasa mapya ambayo mengi hayana vumba vya kujisitiri.


Akijibu swali hilo, Silinde amesema lengo la kujenga vyumba hivyo ni kuwasaidia wanafunzi hao wanapokuwa katika siku zao za hedhi ili wasikose masomo.


“Tunazielekeza halmashauri zote kujenga vyumba ambavyo vitawasaidia hawa watoto kujisitiri wakati wa hedhi, lengo ni kuhakikisha hawakosi masomo wakati huo ili kuweza kuwasaidia kama ambavyo katika michoro yetu mipya tumeainisha,”amesema.


Katika swali la msingi, Santiel amehoji Serikali haioni haja ya kujenga vyoo maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika madarasa mapya yanayojengwa ili wanafunzi hawa wasikose masomo pindi wanapokuwa kwenye siku zao.


Akijibu swali hilo, Silinde amesema ujenzi wa matundu ya vyoo unazingatia mahitaji ya wanafunzi wote wakiwemo wavulana na wasichana pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso