MZAZI AUA MWANAE KWA KIPIGO AKIMTUHUMU KUFANYA MAPENZI NA MTOTO WA JIRANI YAKE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 2 November 2022

MZAZI AUA MWANAE KWA KIPIGO AKIMTUHUMU KUFANYA MAPENZI NA MTOTO WA JIRANI YAKE

Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lusikwi wilayani Sengerema, Nyanzila Shome (17) amefariki dunia akidaiwa kupigwa na mzazi wake Jephta Shome aliyekuwa akimtuhumu kufanya mapenzi wa mtoto wa jirani yake.


Mwanafunzi huyo amekumbwa na mauti hayo siku moja kabla ya kuanza mtihani wa kidato cha pili shuleni hapo.


Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Maili Makori amesema wanawasaka wazazi wa mtoto huyo waliotoweka mara baada ya mauaji hayo.


Amesema tukio hili lilitokea Oktoba 30 majira ya usiku, ambapo baba wa mtoto (Jephta Shome) anayeelezwa kuwa na tetesi za mwanaye kutembea na mtoto wa jirani yake, alipofika nyumbani alianza kumushambulia mwanafunzi huyo kwa kipigo, hali iliyosababisha kifo cha mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso