MAKADA WA CHADEMA WALIOHUKUMIWA KWA UBAKAJI WAACHIWA HURU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 16 November 2022

MAKADA WA CHADEMA WALIOHUKUMIWA KWA UBAKAJI WAACHIWA HURU


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imewachiwa huru makada wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya wizi, unyang'anyi wa kutumia silaha na ubakaji.


Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Novemba 16, 2022 na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Athuman Matuma baada ya kuridhika na hoja za warufani kuwa ushahidi uliowatia hatiani Aprili 12, mwaka huu, ulikuwa dhaifu, unaotia mashaka na usiokubalika mbele ya macho ya sheria.


Wana Chadema walitiwa hatiani kwa makosa mawili ya wizi, ubakaji, kuharibu mali na unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kukamatwa wakiwa kituo cha kupigia kura Kata ya Dutwa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu walikokuwa mawakala wa wagombea wa chama hicho kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.


Pamoja na wizi wa Sh300, 000, warufani hao kwa pamoja walidaiwa kumbaka msadizi wa kituo cha kupigia kura ambaye jina lake lilihifadhiwa kulinda utu na heshima yake mbele ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso