MAJADILIANO YA SERIKALI NA BUNGE YAKWAMISHA MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 11 November 2022

MAJADILIANO YA SERIKALI NA BUNGE YAKWAMISHA MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ambao ulikuwa ujadiliwe bungeni leo Ijumaa na kukamilisha hatua zote tatu, umeahirishwa hadi hapo mashauriano kati ya Bunge na Serikali yatakapokamilika.


Akizungumza leo Novemba 11, 2022 Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema kuna mambo ambayo hawajaafikiana na Serikali hivyo umeondolewa katika ratiba ya shughuli za leo ambapo Bunge linaahirishwa.


Amesema katika orodha ya shughuli za Bunge za leo kulikuwa na hati za kuwasilishwa mezani na kwamba hati hizo zilitakiwa kuwasilishwa na Waziri wa Afya na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.


“Sasa hati hii haitawasilishwa leo mezani kwasababu Bunge pamoja na Serikali tunaendelea na mashauriano juu ya mambo ambayo hatujaafikiana vizuri,”amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso