HAKIMU ADAIWA KUJIUA KWA KUNYWA SUMU - SUMBAWANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 29 November 2022

HAKIMU ADAIWA KUJIUA KWA KUNYWA SUMU - SUMBAWANGA

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Michael Royan (31) anadaiwa kujiua kwa kunywa sumu katika nyumba ya kulala wageni ya ‘gesti’ iliyopo Manispaa ya Sumbawanga mkoani humo.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumanne Novemba 29, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Theopista Mallya amesema tukio hilo limetokea Novemba 27 mwaka huu akiwa amelala katika nyumba ya wageni.


Amesema kuwa asubuhi ya siku hiyo ofisa upelelezi wa mkoa wa Rukwa alipigiwa simu na mmiliki wa nyumba hiyo na kueleza kuwa kuna mteja ambaye amelala na hajaamka na inaonekana kuwa amepoteza fahamu.


Kamanda Mallya amesema baada ya polisi kufika eneo hilo waliingia ndani ya chumba hicho na kumchukua mtu huyo kisha kumpeleka hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Sumbawanga ambapo alipokelewa na baada ya uchunguzi wa awali wa kitabibu ilibainika kuwa mtu huyo amefariki dunia.


Amesema kuwa Polisi walipoanza uchunguzi wa tukio hilo walibaini kuwa marehemu alikua ni mtumishi wa Serikali katika idara ya mahakama mkoani hapa katika mahakama ya mwanzo na kituo chake kilikuwa ni Mahakama ya mwanzo Kasanga.


Kwa habari zaidi tembelea tovuti 

https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/hakimu-adaiwa-kujiua-gesti-sumbawanga--4037196

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso