TAZAMA PICHA ZA TAMASHA LA WARAGHBISHI CHINI YA TWAWEZA-DAR ES SALAAM - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 5 October 2022

TAZAMA PICHA ZA TAMASHA LA WARAGHBISHI CHINI YA TWAWEZA-DAR ES SALAAM

SHIRIKA lisilo la kiserikali la TWAWEZA linalojishughulisha na miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jamii ikiwemo ya kilimo kwa kushirikiana na wananchi wenye kiu ya maendeleo (WARAGHBISHI) limewakutanisha kwa pamoja viongozi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam katika Tamasha maalum la WARAGHBISHI.

 

Tamasha hilo lililoanza leo Oktoba 05, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa APC jijini Dar es salaam lina lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii au wananchi namna ya upatikanaji wa taarifa muhimu zinazohusu maendeleo ambapo Tamasha hilo litafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo Oktoba 05 hadi Oktoba 7, 2022.

 

Pia Tamasha hilo linalenga kuwakumbusha wananchi katika ushiriki wao katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na washiriki wa Tamasha hilo ni viongozi wa dini, maafisa maendeleo na wananchi kutoka mikoa ya Lindi, Kigoma, Simiyu, Dar es salaam, Geita, Tanga, Shinyanga na Simiyu.































No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso