MZEE WA MIAKA 90 NA WATOTO WAKE WATATU WATUHUMIWA KWA MAUAJI YA NDUGU YAO, KISA ALISHIRIKI KIKAO CHA FAMILIA AKIWA AMELEWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 28 October 2022

MZEE WA MIAKA 90 NA WATOTO WAKE WATATU WATUHUMIWA KWA MAUAJI YA NDUGU YAO, KISA ALISHIRIKI KIKAO CHA FAMILIA AKIWA AMELEWA



Mzee mwenye umri wa miaka 90 na wanawe watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya ndugu yao wakimtuhumu kushiriki kikao cha usuluhishi akiwa amelewa.


Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza watuhumiwa hao wanadaiwa kumwadhibu ndugu yao kwa kumchapa kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili, wakimtuhumu kuwaaibisha kwa kushiriki kikao cha usuluhishi akiwa amelewa.


Ndugu hao wanaoshikiliwa na polisi wakituhumiwa kumuua ndugu yao, Simon Leshoo (35) ni Leshoo Kisoki Mollel (90) ambaye ni baba mzazi na wanawe, Simon Leshoo (30), Baraka Leshoo (38) na Abedi Leshoo (15), wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Munge wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro.


“Jamaa ni mpiga maji sana, sasa tunavyosikia kulikuwa na kikao cha usuluhishi, sijajua ni cha ndugu au kilihusisha pia na watu wengine nje ya familia. Hiyo siku jamaa alikuja yuko tungi (amekunywa) na iliwaudhi ndugu,” chanzo kilichokataa jina lake kuandikwa gazetini kilidai.


Chanzo hicho kimedai kuwa kitendo hicho kilimkera baba yake pamoja na ndugu wengine na ndipo walipokubaliana kumwadhibu kama njia ya kumuonya asirudie kufanya kitendo cha aina hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso