MWANAFUNZI DARASA LA TANO AJINYONGA NYUMA YA MLANGO NYUMBANI-SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 28 October 2022

MWANAFUNZI DARASA LA TANO AJINYONGA NYUMA YA MLANGO NYUMBANI-SHINYANGA



MWANAFUNZI wa darasa la tano shule ya msingi Ndala ‘A’ Manispaa ya Shinyanga Bryton Daniel (11) amekutwa amejinyonga kwa kamba nyuma ya mlango nyumbani kwao.


NA HALIMA KHOYA-HUHESO DIGITAL SHINYANGA


Tukio hilo limetokea Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 4 asubuhi, nyumbani kwao Mtaa wa Mwabundu Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.


Akielezea tukio hilo jana mama mkubwa wa marehemu Joyce Kalulu, alisema mtoto huyo hakuwa hana tatizo lolote, lakini siku hiyo walipomaliza kunywa chai, yeye aliondoka kwenye mihangaiko yake ya maisha na aliporudi nyumbani majira ya saa 8 mchana akakuta mlango umefungwa kwa ndani, walipovunja wakamkuta kijana wao amejinyonga.


“Asubuhi nimeamka na kufanya kazi zote nikawa nimewaacha kijana wangu na bibi yake, nimerudi saa 8 kutoka kazini nikamkuta mama anahangaika kumuita Brayton afungue mlango, ndipo tulipoamua kwenda kumuita Mwenyekiti ambaye alifanikiwa kutoboa nyavu za dirisha na kumuona Brayton akiwa amening’inia mlangoni,”alisema Kalulu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwabundu Pili Masanja alisema taarifa za tukio hilo alizipata majira ya saa 9 mchana, na alipofika kwenye familia hiyo ikabidi watoboe nyavu ya dirisha alipochungulia akamuona mtoto huyo akiwa amejinyonga nyuma ya mlango.


“Majira ya saa 9 nilikuja kuitwa na Joyce Kalulu ili nikawasaidie kufungua mlango ambapo nilizunguka nyuma yumba ili kutoboa dirisha lakini tulichokiona baada ya kutoboa dirisha ni Brayton akiwa amejinyonga na kamba nyeusi kwenye mlango, ndipo nikapiga simu Polisi,”alisema Masanja.


Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa Shinyanga Janeth Magomi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha kuwa Jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi ili kubainisha chanzo cha tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso