AUAWA KWA KUKATWA NA MAPANGA AKIWA ANAMUOGESHA MJUKUU WAKE, WANANCHI WAFUNGUKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 31 October 2022

AUAWA KWA KUKATWA NA MAPANGA AKIWA ANAMUOGESHA MJUKUU WAKE, WANANCHI WAFUNGUKA



Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Nshoma Moshi mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa Kijiji cha Mwamalulu Kata ya Didia halmashauri ya Shinyanga ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa mapanga wakati akimuogesha mjukuu wake majira ya saa mbili usiku akiwa nyumbani kwake.


NA HALIMA KHOYA- HUHESO DIGITAL- SHINYANGA


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi amesema tukio hilo limetokea Oktoba 29 mwaka huu katika kijiji cha Mwamalulu Kata ya Didia.


Amesema chanzo cha mauaji hayo kikidaiwa kuwa ni ugomvi wa mashamba baada ya mwanamke huyo kushinda kesi mahakamani na kukabidhiwa mashamba yake huku aliyekuwa wakidaiana mashamba ametoroka baada ya kutokea kwa tukio hilo.


Kufuatia matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi, kamanda Magomi amewataka wananchi kufuata sheria badala ya kusababisha mauaji ya watu wasiokuwa na hatia ambayo yangemalizwa kwa kushirikisha vyombo husika.


"Tukio la mauaji lililotokea oktoba 29 2022 majira ya saa 2 usiku kijiji cha mwamalulu Kata ya Didia Wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo mwana mama mwenye umri wa miaka 50 Nshoma Moshi, ameuliwa kikatili na watu wasiofahamika, Nawaomba wananchi wote watoe taarifa ili kuwabainisba wahusika waliohusika na mauaji haya"Amesema Magomi.


pia nawaomba wananchi wote kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani vyombo husika vitashughulika na yeyote anayevunja sheria,na siyo kufanya mauaji"Ameongeza.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamalulu,Senga Shimba amesema matukio ya mauaji kuanza kutokea katika kijiji hicho yamewashitua huku akiomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini waliohusika kumuua mama huyo kwa kumkata mapanga.


Nao baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwamalulu wamesema kuwa tukio hilo nilakusikitisha kwa kua mama huyo ameuawa kikatili ambapo wamemkata kwa mapanga haki iliyopelekea kifo chake,tunaomba Jeshi la Polisi lifanye chunguzi wa kina ili kuweza kutoa funzo kwa watu wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso