ALIEMKASHIFU RAIS SAMIA KWENYE WHATSAPP AHUKUMIWA MIAKA SABA JELA NA FAINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 21 October 2022

ALIEMKASHIFU RAIS SAMIA KWENYE WHATSAPP AHUKUMIWA MIAKA SABA JELA NA FAINI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Sh15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.


Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga ambapo alieleza kuwa mtuhumiwa alitoa taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya Mwaka 2015.


Katika taarifa iliyotolewa Wakili wa Serikali Daniel Masambu imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo katika Jukwaa la Mtandao wa Whatsapp la "Simiyu Breaking News".


Ameeleza kuwa shtaka la kwanza na la pili alitenda Desemba 03 na 04, 2021 mtuhumiwa huyo aliandika kwenye jukwaa hilo maneno ya kumkashifu Rais Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso