WILLIAM RUTO KUAPISHWA JUMANNE BAADA YA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA UCHAGUZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 5 September 2022

WILLIAM RUTO KUAPISHWA JUMANNE BAADA YA MAHAKAMA KUTUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA UCHAGUZI




Rais mteule wa Kenya, William Ruto ataapishwa Jumanne Septemba 13, 2022.


Hiyo ni baada ya Mahakama ya Juu nchini Kenya kutupilia mbali maombi ya kikatiba yalifunguliwa na Raila Odinga kupinga ushindi wa Ruto.


Akitoa uamuzi huo leo Jumatatu Septemba 5, 2022, Jaji Mkuu Martha Koome amesema Raila na waleta maombi wenzake wameshindwa kuthibitisha kuwa kulikuwa na udanganyifu na uchakachuaji wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi, siku na baada ya kupiga kura.


Odinga (77), mwanaisasa mkongwe ambaye aligombea huku akiungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta amepinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9, akiyaita ‘upotoshaji.’


Alishindwa na Ruto kwa kura 230,000 tu chini ya asilimia mbili tu alizohitaji


Uamuzi huo unamfanya Ruto kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya kufuatia uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso