MAKAMU MWENYEKITI CCM ATEMBELEA SHAMBA LA MBEGU LINALOMILIKIWA NA GLOBAL AGENCY LIMITED,AWATAKA WAWEKEZAJI WENGINE KUIGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 4 September 2022

MAKAMU MWENYEKITI CCM ATEMBELEA SHAMBA LA MBEGU LINALOMILIKIWA NA GLOBAL AGENCY LIMITED,AWATAKA WAWEKEZAJI WENGINE KUIGA




MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM),Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana,akiwa ziarani mkoani Kagera kukagua uhai wa chama na Ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025,mojawapo ya sehemu alizotembelea ni shamba la mbegu linalomilikiwa na mwekezaji wa ndani,Missenyi Global Agency,lililoko katika kijiji cha Buchurago,kata ya Bugorora wilayani Missenyi.


Na Mutayoba Arbogast-Huheso digital-Bukoba


Amefurahishwa na utendaji kazi katika shamba hilo la uzalishaji mbegu,na pia uwezo wa vifaa vinavyotumika katika uzalishaji,huku akiwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuja Kagera kuwekeza kwani zipo fursa tele na mazingira ni rafiki.


Winifrida Bashasha,mkurugenzi katika kampuni hiyo amesema lengo lao ni kukabiliana na uhaba wa mbegu zenye sifa,ili taifa liweze kujitosheleza na hata kuuza nchi za nje.


Amesema wanalima mahindi kwa kiasi kikubwa,na pia soya na ngano na kuwa wateja wao wakubwa wa mbegu za mahindi ni Seed Company na Seedland Tanzania.


Amesema kuwa,kuna mahitaji makubwa ya mbegu,lakini changamoto ni kuwa,kwa uchanga wao, hawajalitosheleza soko,matumaini ni kuwa kwa uwekezaji wanaoufanya wa kupanua ukubwa wa shamba kutoka ekari 1,360 ambazo sasa zimelimwa na kupandwa,wana matarajio ya kufikia uzalishaji zaidi ya asilimia 25 kwa miaka mitatu ijayo.


"Kuna uhaba mkubwa wa mbegu hapa nchini,hivyo sisi tuliichukulia kuwa ni fursa ili kusaidiana na serikali na wadau wengine kukabiliana na tatizo hili",amesema Bashasha.


Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo,Fidelis Bashasha amemshukuru Kinana kwa kutembelea shamba hilo,huku akiishukuru serikali kwa jinsi inavyowaunga mkono katika adhma yao ya kuwapatia wananchi mbegu bora,huku akiwaomba wadau wengine kuendelea kuiunga mkono kampuni katika kufikia malengo yake.


Makamu mwenyekiti amefuatana na Shaka Hamdu Shaka,Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na uenezi,na viongozi wengine wa chama na serikali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso