MAKADA CHADEMA WALIOKUWA WANAANDAA UWANJA WA MKUTANO WAKAMATWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 4 September 2022

MAKADA CHADEMA WALIOKUWA WANAANDAA UWANJA WA MKUTANO WAKAMATWA




Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linadaiwa kumkamata Katibu wa Chadema wilaya ya Nyamagana, David Nyakimwe na mwanachama mwingine wa chama hicho, Oswald Mang'ombe wakati wakiendelea na maandalizi ya mkutano wa hadhara uliotarajiwa kufanyika uwanja wa shule ya msingi Mabatini jijini Mwanza.


Akizungumza leo Jumapili, Septemba 4, 2022 na Mwananchi Digital kwa simu, Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zakaria Obadi amesema wanachama hao wamekamatwa asubuhi ya leo wakiendelea na maandalizi ya eneo ulipotakiwa kufanyika mkutano huo.


Obadi amesema pamoja na kutoa taarifa Ofisi ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya Nyamagana kwamba mkutano huo utafanyika leo katika viwanja vya shule hiyo lakini anashangaa kuona jeshi hilo linawakamata wanachama wake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso