MABALOZI WATAKIWA KUHAMASISHA UPATIKANAJI WA MAZOKO YA NDANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 20 September 2022

MABALOZI WATAKIWA KUHAMASISHA UPATIKANAJI WA MAZOKO YA NDANI



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania, katika mataifa mbalimbali waweke msisitizo katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi na kuhamasisha zaidi upatikanaji wa masoko wa bidhaa za ndani na uwekezaji.


Waziri Mkuu amesema hayo alipokutana na mabalozi hao ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma, ambao ni Balozi aliokutana nao ni Balozi Caroline Chipeta (Uholanzi), Balozi Simon Sirro (Zimbabwe) na Balozi Luteni Jenerali Mathew Mkingule (Zambia).


"Nchi yetu ni moja kati ya mataifa ambayo jiografia yake imekaa kimkakati, tuna masoko kutoka jumuiya mbalimbali ikiwemo SADC na EAC, hata mazingira yetu ya uwekezaji ni mazuri, tunazo ndege, bandari na sasa tunaendelea kufanya maboresho makubwa kwenye sekta ya nishati," amesema Waziri Mkuu


"Nendeni mkatafute masoko ya bidhaa zetu za ndani, shirikini kwenye maonesho yanayoandaliwa ili mtangaze bidhaa zetu, tunataka wakulima wetu wanufaike kwa kupata masoko kutoka kwenye nchi mnazokwenda," ameongeza Waziri Mkuu.


Aidha waziri Mkuu amesema Tanzania inahitaji wawekezaji makini watakowekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, madini na maliasili. "Tunataka uwekezaji wenye tija ili kuimarisha uchumi wetu, pia tunataka wawekezaji watakaozalisha bidhaa hapa nchini kwa kutumia malighafi zetu,".


Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewasisitiza mabalozi hao wahakikishe wanalinda taswira ya Tanzania katika nchi uwakilishi sambamba na kujielekeza katika kuvutia watalii na kuwasaidia wafanyabiashara wa Kitanzania kufanya biashara nje.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso