TOZO ZA MABENKI ZAFUTWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 20 September 2022

TOZO ZA MABENKI ZAFUTWA



Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba

Serikali imefuta tozo ya miamala ya kielektroniki ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu na miamala ya simu kwenda benki.


Hayo yamebainishwa hii leo Septemba 20, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, na kusema punguzo la tozo hizo litaanza kutumika Oktoba Mosi mwaka huu.


"Marekebisho yanayotarajiwa kufanyika ni kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote, kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na ile ya kwenda benki moja kwenye nyingine, kutowahusisha wafanyabishara kama ilivyuokuwa kwenye kanuni za sasa, kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia ATM," amesema Waziri wa fedha

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso