ACT-WAZALENDO YAPITISHA MAJINA WAGOMBE UBUNGE WENGI KURA ZIMEPUNGUA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 4 September 2022

ACT-WAZALENDO YAPITISHA MAJINA WAGOMBE UBUNGE WENGI KURA ZIMEPUNGUA



Kamati Kuu ya ACT-Wazalendo, iliyoketi kwa siku mbili mfululizo imewapitisha Ado Shaibu na Pavu Abdallah kuwania nafasi ya ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala).


Kamati Kuu hiyo iliketi kuanzia Septemba 2 na 3 Jijini Dar es Salaam, ilichagua Shaibu (Katibu mkuu wa ACT-Wazalendo) kwa upande wa Tanzania Bara pamoja na Pavu (Naibu Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu wa CT-Wazalendo) kutoka Zanzibar watakaoipeperusha bendera ya chama hicho, katika Eala.


Katibu wa Katibu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa chama hicho, Mohammed Masaga ameiambia Mwananchi leo Jumapili Septemba 4, 2022 kwamba Shaibu na Pavu walichaguliwa jana Septemba 3, 2022 katika mchakato ulianza saa moja hadi saa tatu usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso