WALIMU WAPIGWA MARUFUKU KUHAMIA MJINI KUTOKA VIJIJINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 13 September 2022

WALIMU WAPIGWA MARUFUKU KUHAMIA MJINI KUTOKA VIJIJINI


Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametoa zuio kwa walimu wa ajira mpya kuhama kutoka maeneo ya vijijini waliopangiwa kazi na serikali kwani kwa kufanya hivyo kumekuwa kikiathiri kiwango cha ukuaji wa elimu hususani maeneo ya vijijini


Mkuu wa Mkoa amesema hayo wakati akikabidhi vitabu vya mwongozo wa namna ya ufundishaji ambapo mkuu wa mkoa amesema kuwa kumekuwa na tabia ya walimu kupewa ajira na serikali na baadaye kuanza kuomba kuhamia mijini kwa sababu ambazo hazina mashiko


Katika Kikao hicho pia mkuu wa mkoa amesikiliza kero mbalimbali zinazowakabiri wananchi na kahidi kuzifanyia ufumbuzi.


Afisa elimu mkoa wa Njombe mwalimu Neras Aron Mulungu amesema kuwa wananchi mkoani Njombe wamefanya kazi kubwa kujenga nyumba za walimu huku akisema tabia ya walimu kukimbilia mijini inatokana na huruka ya mtu binafsi huku akisema kwa sasa huduma zote zilizopo mjini kama umeme zimefikishwa mpaka vijijini.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso