WILLIAM RUTO AAPISHWA KUWA RAIS WA KENYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 13 September 2022

WILLIAM RUTO AAPISHWA KUWA RAIS WA KENYA



William Ruto, Rais wa Tano wa Taifa la Kenya, wakati akila kiapo


William Ruto ameapishwa rasmi kuwa rais wa tano wa Kenya . Ruto alikula kiapo siku ya Jumanne , Septemba 13 katika uwanja wa Moi Kasarani katika sherehe iliosimamiwa na msajili wa idara ya mahakama Anne Amadi na kushuhudiwa na jaji mkuu Martha Koome .


Mkewe Mama Rachel Ruto alikuwa amesimama kando yake wakati akila kiapo hicho.


“Mimi, William Samoei Ruto, kwa kutambua kikamilifu wito wa juu ninaochukua kama Rais wa Jamhuri ya Kenya, naapa kwamba nitakuwa mwaminifu wa kweli kwa Jamhuri ya Kenya, aliapa rais mpya William Ruto.


Martha Koome baadaye alimwalika rais anayeoondoka madarakani Uhuru Kenyatta, akiandamana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Kenya Jenerali Robert Kibochi kumkabidhi zana za mamlaka - Upanga wa Heshima na Katiba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso