WATUMISHI 18 WA KATA NA VIJIJI WAFUKUZWA KAZI SINGIDA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 4 August 2022

WATUMISHI 18 WA KATA NA VIJIJI WAFUKUZWA KAZI SINGIDA



Watumishi 18 wa halmashauri ya Iramba mkoani Singida ambao ni Watendaji wa Kata na Vijiji wamefukuzwa kazi kufuatia kushindwa kurejesha shilingi milioni 364 ambazo ni fedha za mapato ya ndani.


Watumishi hao ni kati ya 20 wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kati ya 52 waliotuhumiwa kukusanya mapato zaidi ya Milioni 353 na kushindwa kuziingiza kwenye mfumo wa mapato wa halmashauri.


Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungunza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Julai 21, 2022 alisema baada ya maagizo ya Waziri Mkuu, kuliundwa kamati ya kuchunguza kero zilizolalamikiwa na wananchi likiwamo suala la fedha.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofanya ziara wilayani Iramba Julai 16, mwaka huu wananchi wa mji wa Misigiri waliandika mababgo kadhaa ya malalamiko wakilalamikia utendaji kazi wa baadhi ya watumishi.

CHANZO: ITVINSTAGRAM

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso