RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 4 August 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI TBC

 

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bwana Erick Benedict Hamissi kuwa mkurugenzi wa kampuni ya huduma za meli (MCL) ambapo kabla ya uteuzi huo Bwana Hamissi alikuwa mkurugenzi wa Bandari Tanzania (TPA).

 

Wakati huo huo, Mhe. Rais Samia amemteua Bw. Stephen Nzohabonayo Kagaigai kuwa mwenyekiti wa bodi ya Shirika la utangazaji Tanzania (TBC) ambapo Bwana Kigaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbert E. Mrango ambaye amemaliza kipindi chake.

 

Taarifa ya mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema kuwa uteuzi huo umeanza mara moja.

CHANZO:IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso