WAFUASI WA CHADEMA WALIOKABILIWA NA MAUAJI WAACHIWA HURU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 5 August 2022

WAFUASI WA CHADEMA WALIOKABILIWA NA MAUAJI WAACHIWA HURU


Aliyekuwa diwani wa Kata ya Isengule Mkoani Katavi Ocsar Sangu na wenzake watano ambao ni wafuasi wa CHADEMA waliokaa mahabusu kwa miaka minne wameachiwa huru baada ya kubainika hawana hatia


Walikuwa wanakabiliwa na tuhuma za kuwaua wafanyabiashara waliokuwa wakinunua mazao katika Kijiji Chao.


Bwana Ocsar Sangu ambaye ndiye alikuwa Diwani wa Isengule na wenzake baada ya kuachiwa huru walikimbilia kanisa katoliki na kufanya ibada kabla ya kwenda nyumbani kuzungumzia halisi halisi ilivyokuwa mpaka wao kujikuta kwenye mikono ya sheria.


Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Ndg Isaya Kalimwabu amezishukuru mamlaka husika kwa kutenda haki.


Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Katavi wameendelea kuiomba Serikali kutenda haki na kuweka kando mambo ya siasa na vyombo vya ulinzi na usalama,huku wakisisitiza siasa uwe ni mchezo kipindi Cha uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso