OMBI LA MBUNGE LAGONGA MWAMBA KWA RAIS SAMIA SERIKALI IMEJIELEKEZA KUPELEKA HUDUMA SIO KUKATA MAENEO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 5 August 2022

OMBI LA MBUNGE LAGONGA MWAMBA KWA RAIS SAMIA SERIKALI IMEJIELEKEZA KUPELEKA HUDUMA SIO KUKATA MAENEO



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake haina mpango wa kukata maeneo kwa kuyapandisha hadhi, badala yake wanajielekeza kwenye utatuzi wa shida za wananchi hapa nchini.


Rais Samia ametoa msimamo huo leo Ijumaa Agosti 5, 2022 akiwa Mbalizi mkoani Mbeya baada ya kupokea ombi kutoka kwa mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza la kutaka Mbalizi kupandishwa hadhi na kuwa halmashauri ya mji.


Mbunge huyo alimwomba Rais Samia kuupandisha hadhi mji wa Mbalizi ili uwe halmashauri ya mji akidai kwamba itasaidia kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi wa Mbalizi na maeneo mengine ya jirani.


Akizungumzia jambo hilo, Rais Samia amesema alipokea ombi hilo kutoka kwa viongozi, hata hivyo amewaeleza wananchi wa Mbalizi kwamba Serikali yake imejielekeza kwenye utatuzi wa shida za wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso