UNUNUZI WA LUKU KUPOTEA KWA SIKU NNE-TANESCO YATHIBITISHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 17 August 2022

UNUNUZI WA LUKU KUPOTEA KWA SIKU NNE-TANESCO YATHIBITISHA




Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya Luku kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.


Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Cliff Maregeli amebainisha hayo leo Jumatano Agosti 17, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matengenezo kinga kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.


Amesema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku.


Amewataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa Luku katika kipindi kilichobainishwa.


"Shirika linashauri wateja wake kununua umeme wa ziada au kufanya manunuzi ya umeme nje ya muda wa matengenezo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kazi hii.


"Matengenezo haya muhimu yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku ili kuwahudumia wateja wetu kwa ufanisi zaidi," amesema Maregeli.


Kwa upande wake, Msemaji wa Tanesco, Martin Mwambene amesisitiza kwamba faida kubwa ya matengenezo hayo ni kujihami dhidi ya changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye na matengenezo yakawa makubwa zaidi na kusababisha wananchi kukosa umeme.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso