NJOMBE YAMALIZA KUHESABU WATU-RC ATOA PONGEZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 28 August 2022

NJOMBE YAMALIZA KUHESABU WATU-RC ATOA PONGEZI




Mkoa wa Njombe umemaliza dodoso kuu la sensa ya watu kwa zaidi ya asilimia 100 kabla ya siku zilizopangwa kukamilika.


Sensa ya Watu na Makazi ilianza Agosti 23, 2022 na itakamilika kesho Jumatatu.


Hayo yamesemwa leo Jumapili Agosti 28, 2022 na Mkuu wa Mkoa huo, Anthony Mtaka baada ya kupokea taarifa ya uandikishaji wa sensa ya watu na makazi wilaya Makete.


Amesema halmashauri tano za Mkoa wa Njombe zimekamilisha sensa ya watu na makazi kwa asilimia mia moja hivyo imebakia moja ambayo itamaliza leo.


Amesema mkoa huo kesho asubuhi Jumatatu utakabidhiwa rasmi taarifa kutoka katika halmashauri zote za mkoa wa Njombe za ukamilishaji wa sensa ya watu na makazi.


"Kila halmashauri kesho itakabidhi taarifa rasmi ya ukamilishaji wa sensa na kuweza kupongezana kwamba tumemaliza kabla ya wakati kama ambavyo tulitarajia," amesema Mtaka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso