JAJI MTUNGI ATIMULIWE AMESHINDWA KUTATUA MIGOGORO YA CHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 28 August 2022

JAJI MTUNGI ATIMULIWE AMESHINDWA KUTATUA MIGOGORO YA CHAMA


Chama cha NCCR-Mageuzi, upande wa Mwenyekiti James Mbatia umemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumfuta kazi Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakidai inashindwa kutekeleza majukumu yake kwa weledi ikiwamo kusuluhisha mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho.


Chama hicho kimegawanyika katika pande mbili wa Mbatia na ule unaomuunga mkono makamu Mwenyekiti Zanzibar, Ambar Khamis uliojitokeza kufuatia kikao kilichofanyika Mei 21, 2022 maeneo ya Kurasini na kutangaza kuwasimamishwa baadhi ya viongozi akiwamo Mbatia kwa makosa ya kugombanisha viongozi wenzao.


Upande huo umesema kitendo cha ofisi hiyo kushindwa kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene Agosti 15, 2022 yaliyowataka kumaliza mgogoro unaowatafuna kwa zaidi ya miezi mitatu kwa kuzingatia katiba ya chama hicho ni wazi amekosa sifa ya kubakia katika nafasi hiyo.


Hata hivyo, Jaji Mutungi amekiri kupokea maagizo ya Waziri kwa barua huku akidai ukimya wake juu ya mgogoro huo si kwamba ameshindwa kusuluhisha, isipokuwa alikuwa anafanya maandalizi kisha awatumie wito wa kuwaita kwenye kikao cha pamoja kuzungumzia suala hilo.


“Nashangaa kwenye mkutano wao badala wanitake niharakishe kuwaita wao wanaanza kunishambulia lakini wanapaswa kutambua ofisi yangu inafanya shughuli zake kwa kuzingatia utaratibu si kama wanavyofikiri wao,” amesema Jaji Mutungi


Akizungumza leo Jumapili Agosti 28, 2022 katika mkutano wao na vyombo vya habari, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa NCCR Mageuzi, Samwel Ruhuza amesema wanawasiwasi na uwezo wa Jaji Mtungi na kushindwa kuisimamia ofisi hiyo vyema kunaondoa uhalali wa kuendelea kubakia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso