NEEMA WA MFALME ZUMARIDI AANGUKA KIZIMBANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 31 August 2022

NEEMA WA MFALME ZUMARIDI AANGUKA KIZIMBANI



 
Kesi namba 12 inayomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi, na wenzake 84 ya kufanya mkusanyiko usio halali imelazimika kusimama kwa muda wa nusu saa baada ya mshtakiwa namba 74 aitwaye Neema Juma kuanguka akiwa kizimbani.


Mshtakiwa huyo namba 74 aitwaye Neema Juma, ameanguka mbele ya Mahakama wakati shahidi Deonice John ambaye ni mjumbe wa serikali ya mtaa wa Buguku Buhongwa, alipokuwa akitoa ushahidi wake ndipo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza Clesensia Mushi, akiahirisha kesi hiyo kwa muda wa dakika 30.


Baada ya mapumziko hayo ya muda mfupi Mahakama ilirejea na Wakili upande wa utetezi, Erick Mutta, akalazimika kuomba Mahakama iahirishe kesi hiyo mpaka siku itakayopangwa tena ili mahakama na magereza waone namna ya kumpatia matibabu mtuhumiwa huyo.


Aidha, kwa upande wa Wakili wa serikali mwandamizi, Dorcas Akyoo, akaiomba Mahakama mshatakiwa huyo namba 74 apewe dhamana ili aweze kufanyiwa matibabu kwa uhuru kutokana na kesi inayomkabili kuwa na dhamana huku upande wa utetezi ukiiomba mahakama iangalie kama mshtakiwa huyo hajakidhi vigezo afutiwe mashtaka.


Kesi hiyo inayoongozwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza, Clescensia Mushi imeahirishwa hadi Septemba 13, mwaka huu ili mshtakiwa huyo aweze kupata matibabu.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso