MIKOA YA DAR NA PWANI INA MANABII WA UONGO WASAKA FEDHA ZA WATU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 7 August 2022

MIKOA YA DAR NA PWANI INA MANABII WA UONGO WASAKA FEDHA ZA WATU



Mkuu wa jimbo la kati Dayosisi ya Magharibi Kati wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Baraka Mungure amedai mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ina baadhi ya manabii ni waongo na wanasaka fedha za watu badala ya kuponya mioyo yao.


Mungure ametoa kauli hiyo leo Jumapili Agosti 7, 2022 wakati akihubiri kwenye ibada ya kwanza ya katika kanisa la Azania Front mkoani Dar es Salaam.


Kabla ya kutoa ujumbe huo, mahubiri yake yalijengwa katika msingi wa maagizo ya Mungu kupitia biblia takatifu, Yeremia sura 23:16-22 (waumini wa Kikristo), ujumbe unaosema; Bwana wa Majeshi asema hivi, msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria, kuwafundisha ubatili, hunena maono ya mioyo yao, ambayo hayakutoka katika kinywa cha bwana. 


Tazama tufani ya bwana, yaani ghadhabu yake imetokea, ni dholuba ya kisulisuli, itapasuka na kuwaangukia waovu kichwani. Hasira ya bwana haitarudi. 


Siku za mwisho mtalifahamu hilo neno, mimi sikuwatuma manabii hao lakini walikwenda mbio, sikusema nao lakini walitabiri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso