WAPANGAJI KULIPA ASILIMIA KUMI YA PANGO TRA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 25 August 2022

WAPANGAJI KULIPA ASILIMIA KUMI YA PANGO TRA

 

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesisitiza wapangaji katika nyumba za kapanga kuwa wazalendo na kulipia asilimia 10 ya kodi wanazokuwa wakilipa kwa wenyenyumba ili kulipia kodi ya pango.


Hayo yamesemwa na Ofisa Huduma na Elimu Mkuu wa TRA, Eugenia Mkumbo katika mafuzo ya wafanyabiashara juu ya mabadiliko ya sheria ya kodi mwaka 2022, leo Alhamisi Agosti 25, 2022 wilayani Bariadi, Mkoa wa Simiyu.


Amesema kifungu cha 82(2) (a) cha sheria ya kimefuta msamaha wa kodi kwa wapangaji binafsi, hivyo kuwapa mamlaka wapangaji wote kuzuia kodi ya pango katika nyumba binafsi na zile za biashara ili kurahisisha ulipaji na ukusanyaji wa kodi ya pango.


"Kama umepanga chumba kiwe cha biashara au makazi unajukumu la kukata asilimia 10 na kuilipa TRA na mwenye nyumba utampelekea nakala ambayo inaonyesha umelipia kodi, utaambatanisha na pesa iliyobaki unampa mwenye nyumba," amesema Eugenia

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso