MBARONI KWA KUMUU BABA YAKE MZAZI KISA UNYUMBA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 25 August 2022

MBARONI KWA KUMUU BABA YAKE MZAZI KISA UNYUMBA




Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara, linamshikiliaHamisAthumani (23), Makazi wa Chingungwe, wilayani Tandahimba kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi, Hamis Chimpota (50).


Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema tukio hilo limetokea jana Jumatano Agosti 24, 2022, saa 12:00 jioni, katika Kijiji cha Chingungwe.


Amesema mtuhumiwa huyo alimpiga baba yake kichwani eneo la kisogoni kwa kutumia kipande cha mti.


"Mtuhumiwa alitenda kosa hilo kutokana na ugomvi wa kifamilia uliozuka baada ya mtuhumiwa kutoridhika na maelekezo ya wazazi wake kwamba aache tabia ya kuomba unyumba kwa mkewe mwenye kitoto kichanga," amesema Katembo.


Kamanda huyo amesema, mwili wa Chimpota umehifadhiwa ukisubiri uchunguzi wa daktari.


Aidha, Jeshi hilo linaendela na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso