MAMA ALIYEKIMBIA WATOTO KISA MWANAUME AJISALIMISHA POLISI NA KUOMBA KURUDI KUWALEA WATOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 3 August 2022

MAMA ALIYEKIMBIA WATOTO KISA MWANAUME AJISALIMISHA POLISI NA KUOMBA KURUDI KUWALEA WATOTO

 


MAMA wa watoto watatu wakike Mkazi wa kijiji cha Gombe tarafa ya Mwaya, wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Adelyda Nakashawa amejisalimisha kituo cha polisi na kuomba kurudi kuwalea watoto wake baada ya kuewatekeleza kwa wanawe tangu mwaka 2017 kisa mwanaume.


Mama huyo alijisalimisha Agosti 1, mwaka huu (2022) baada ya kuona taharuki kwa muda mrefu na Polisi wilayani Ulanga wakiendelea kumtafuta na yeye kuhama kila eneo alipokimbilia kujificha.


Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Ngolo Malenya alisema hayo jana mjini Morogoro kuwa mama huyo aliona ajisalimishe baada ya kupata taarifa ya kwamba bado anaendelea kutafutwa na polisi kwa agizo la mkuu wa wilaya.


Wazazi wote wawili waliondoka nyumbani kwao tangu mwaka 2017 na kuwatekeleza watoto hao wakike akitangulia mwanamke kuolewa na mume mwingine na kufuatia mume kuoa mke mwingine.


“Baada ya agizo langu la kukamatwa kwa wazazi waliotelekeza watoto mama yao Adelyda Nakashawa amejisalismisha polisi, lakini mpaka sasa Thomas Ulanda baba mzazi wa watoto hao anaendelea kutafutwa na polisi” alisema Malenya.


Mkuu wa wilaya alisema baada ya kujisalimisha kwake aliviagiza vyombo vya sheria vifanye jukumu lake.


Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya huyo kuwa , mama huyo alijieleza kuwa aliposhindana na mume wake wa kwanza Thomasi Ulanda, aliolewa na munme mwingine Abdulaziz Kondo ambaye walianza maisha mengine na tayari wana mtoto wa miaka mitatu.

CHANZO:HABARI LEO

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso